Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana.
Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha.
Ngoja nikwambie kitu, asilimia kubwa sana ya vijana wanaomakiza elimu ya chuo au chuo kikuu hawana ujuzi au uwezo wa kuandaa wasifu binafsi yaani C. V na hali hii huwapa vijana hao wakati mgumu pale wanapotafuta ajira iwe ya muda mfupi au mrefu (full time). Vijana wengine hutoa fedha eti kuandikiwa C.V!!!! Inasikitisha sana maana wapo Mpaka walio makazini tena wana uzoefu wa miaka mingi lakini hawana written curriculum vitae wakijisifu na lile wakichonacho kichwani. Hii ni aibu kubwa sana.
Hakuna kitu rahisi kama kuandaa C.V yako binafsi na wataalamu tunashauri ni vyema kuwa unaiboresha ( update) Mara kwa Mara ili kuifanya iwe ya kisasa zaidi. Ikiwa hujajua kuandaa C.V yako ama unajua na huja-update usijali kwa sababu kupitia makala hii najua utakuwa na uwezo wa kuandika wewe mwenyewe na utafurahia.
Kwanza nini maana ya wasifu binafsi ama Curriculum vitae (C.V)? Hii ni taarifa fupi iliyo rasmi juu ya mtu, sifa, ujuzi na uzoefu wake kitaaluma na kifani. Mara nyingine huitwa "course of life". Wasifu binafsi hukamilisha taarifa zako ikiwa umeandika wa usahihi. Kwa kawaida huandikwa katika karatasi moja au mbili (inaweza kuzidi) ili utumie maneno machache yenye kukamika.
Kwa wenzetu wa marekani hutumia resume ambayo huwa ni fupi zaidi na huandikwa kulingana na kazi unayoomba lakini inayopendekezwa ni Curriculum vitae (C.V). Hii ndiyo maana unapaswa kuwa nayo hard copy na soft copy ili kujiweka tayari wewe kama msomi unayeendana na wakati. Huweza kuandikwa kwa lugha ya kiingereza ama kiswahili itategemea na mahitaji husika.
Ebu ngoja tuangalie vipengere muhimu unapotaka kuandika C. V yenye ushindani katika soko la biashara:
1. Personal Particulars. (Taarifa binafsi)
Hii ni sehemu ya awali kabisa katika uandishi wa C.V yako. Katika sehemu hii taarifa binafsi huitajika nazo huandikwa kwa kufuata mtiririko wa kushuka chini (nitatoa mfano baada). Taarifa hizo ni pamoja na Full name, Sex, Marital status, Current Address, Nationality, Date of birth, Phone number, E-mail Address etc. Sehemu hii utatoa taarifa zote za msingi zinazokuhusu wewe tu. Zingatia taarifa hizo ni sharti ziandikwe kwa ufupi
Itaendelea...
Ushauri... 0756775148