HATIMAYE AMEOLEWA. Kwa miaka zaidi ya kenda, urafiki tuliukoleza Japo mbali nikaenda, pesa kuitafuta Muheza Mupenzi alijilinda, nami penzi nikatunza Leo nalia mwenyewe, hatimaye ameolewa Ahadi tulitukuza, penzi tusije livunja Maneno yake yalinikuza, kama samaki alinikunja Moyo huba alinuiza, Muheza buzi sikuonja Leo nalia mwenyewe, hatimaye ameolewa Simu na jumbe mahabuba, zilinipata si haba Hata sikuwaza suluba, kwa kazi zilizonikaba Nami moyo ulinijaba, nikamwekeza hadi baba Leo nalia mwenyewe, hatimaye ameolewa. Mara wiki ikakatika, mupenzi hapatikani Moyo nikajipa rika, labda simu matatani Hata mwezi ukavunjika, Sina taarifa abadani Leo nalia mwenyewe, hatimaye ameolewa Nikafuata ushauri, kwa wahenga mashuhuri Nipate vipi saburi, wa moyo sinaye habari Baba kasema ni nzuri, kama nikipanga safari Leo nalia mwenyewe, hatimaye ameolewa Mwaka ulofata julai, nikarudi Shambarai Huku najipa tumai, nenda posa wangu Nai Furaha isiyokinai, kwa moyo wangu jinai Leo nali...
Tujadili fasihi Tujiunze fasihi Tuandike na kufurahi. Maabarayafasihi.