NI SALAMA KENYA. Safari iso ndefu, leo mnaitimiza Kama mbio za sakafu, ukingoni mwamaliza Chagua iloturufu, kwa Kenya yenye mwangaza Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza. Chaguzi ni siku moja, mchague wa moyoni Wala msilete vioja, kuivuruga amani Sote ni ndugu moja, mnachagua rubani Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza. Kwa sala namwomba Mungu, alotuweka duniani Wasitufitini wazungu, Afirika ina amani Uchaguzi mwema wezangu, sisi kwenu majirani Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza. ©UPP2017
Tujadili fasihi Tujiunze fasihi Tuandike na kufurahi. Maabarayafasihi.