Mara ya kwanza nakutana na Monika ilikuwa mwaka 2014 nje ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akiwa analia kwa uchungu huku akisaidiwa na mume wake, monika alionekana kama mtu aliyekata tamaa kwa kukosa msaada. Walitembea taratiba kuelekea upande wa pili wa barabara lakini ghafla nikamwona Monika akianguka chini na mmewe akijaribu kumuinua huku na yeye akitokwa machozi. Ikanibidi niende kuwasaidia na tukaketi kwenye mgahawa jirani ili wapumzike kidogo. Tukiwa hapo nikatamani sana kujua nini hasa kimewasibu ndipo Monika akaanza kunisimulia... "akasema wametoka kufanya checkup ya mfumo wa uzazi na daktari akamwambia hawezi kupata ujauzito katika maisha yake. Nilistuka kidogo lakini akaendelea kusema.... "ameishi na mume wake miaka sita pasipo kupata mtoto, wamejaribu kila aina ya dawa pasipo mafanikio, wameenda kwa waganga wengi lakini bado tatizo halikutatuliwa, wametumia pesa nyingi na hatimaye wakaamua kuja hapo hospitali ndipo wakaambiwa hawezi kupata ujauzito. kwakweli n...
Tujadili fasihi Tujiunze fasihi Tuandike na kufurahi. Maabarayafasihi.