NI SALAMA KENYA. Safari iso ndefu, leo mnaitimiza Kama mbio za sakafu, ukingoni mwamaliza Chagua iloturufu, kwa Kenya yenye mwangaza Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza. Chaguzi ni siku moja, mchague wa moyoni Wala msilete vioja, kuivuruga amani Sote ni ndugu moja, mnachagua rubani Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza. Kwa sala namwomba Mungu, alotuweka duniani Wasitufitini wazungu, Afirika ina amani Uchaguzi mwema wezangu, sisi kwenu majirani Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza. ©UPP2017
'SIJINYIME. NGELEJA©UPP Bandu na bandu kidogo, Utamu wake mkolezo Wala sinipe kisogo, Zidisha kale kamchezo N'kikugusa usiwe mbogo, Njoo upate tulizo Raha ya huba uwazi, Mfichaji ni mwibaji. Niite bebi niitike, nami nikwite laazizi Sura yako isifutike, Moyoni iweke mizizi Unonapo njoo udeke, Walozi uwanyime pumzi Raha ya huba uwazi, Mfichaji ni mwibaji Nikushike utakapo, Nilishe chakula chako Wanojisifu kwa matapo, wamalize kwa kicheko Tuvuke mito mbili popo, nishiriki raha zako Raha ya huba ni wazi, Mfichaji ni mwibaji.