'SIJINYIME.
NGELEJA©UPP
Bandu na bandu kidogo, Utamu wake mkolezo
Wala sinipe kisogo, Zidisha kale kamchezo
N'kikugusa usiwe mbogo, Njoo upate tulizo
Raha ya huba uwazi, Mfichaji ni mwibaji.
Niite bebi niitike, nami nikwite laazizi
Sura yako isifutike, Moyoni iweke mizizi
Unonapo njoo udeke, Walozi uwanyime pumzi
Raha ya huba uwazi, Mfichaji ni mwibaji
Nikushike utakapo, Nilishe chakula chako
Wanojisifu kwa matapo, wamalize kwa kicheko
Tuvuke mito mbili popo, nishiriki raha zako
Raha ya huba ni wazi, Mfichaji ni mwibaji.