Sehemu iliyopita tuliona utangulizi mfupi wa uandishi wa kazi za fasihi na jinsi ambavyo mwandishi alivyoonekana na anavyostahili kuonekana. Ebu Leo tuendelee na sifa za mwandishi anayeendana na Wakati katika kazi yake. Kama tujuavyo, uandishi wa kazi za fasihi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo, mwandishi anapaswa kutambua kwamba taaluma hii haihitaji mchezo . Umakini katika uandishi ndiyo utakuongezea umaarufu ama kukupunguzia, zifuatazo ni sifa baadhi tu ambazo mwandishi anastahili kuwa nazo: 1. Mwandishi anapaswa kuwa ni yule anayeiandikia Jamii anayoifahamu, iwapo utaandika kazi pasipo kuzingatia Jamii yako ama Jamii elekezi basi kazi yako itakosa wasomaji na utapoteza sifa hii ya kuitwa mwandishi 2. Mwandishi ni lazima awe angalau na elimu juu ya uandishi wa kazi za fasihi, ni sifa muhimu sana. Elimu ya uandishi wa kazi za fasihi utakufanya ujue namba ya kupangilia visa na matukio hata Kama ni ya kawaida kiasi gani bado yataonekana ni mkubwa na yakuvutia kwa waso...
Tujadili fasihi Tujiunze fasihi Tuandike na kufurahi. Maabarayafasihi.