Skip to main content

Waandishi na Uandishi.. 2.

Sehemu iliyopita tuliona utangulizi mfupi wa uandishi wa kazi za fasihi na jinsi ambavyo mwandishi alivyoonekana na anavyostahili kuonekana.
Ebu Leo tuendelee na sifa za mwandishi anayeendana na Wakati katika kazi yake. Kama tujuavyo, uandishi wa kazi za fasihi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo, mwandishi anapaswa kutambua kwamba taaluma hii haihitaji mchezo. Umakini katika uandishi ndiyo utakuongezea umaarufu ama kukupunguzia, zifuatazo ni sifa baadhi tu ambazo mwandishi anastahili kuwa nazo:

1. Mwandishi anapaswa kuwa ni yule anayeiandikia Jamii anayoifahamu, iwapo utaandika kazi pasipo kuzingatia Jamii yako ama Jamii elekezi basi kazi yako itakosa wasomaji na utapoteza sifa hii ya kuitwa mwandishi

2. Mwandishi ni lazima awe angalau na elimu juu ya uandishi wa kazi za fasihi, ni sifa muhimu sana. Elimu ya uandishi wa kazi za fasihi utakufanya ujue namba ya kupangilia visa na matukio hata Kama ni ya kawaida kiasi gani bado yataonekana ni mkubwa na yakuvutia kwa wasomaji wako.

 
       Itaendelea..........

          Ushauri.. 0756775148.

Popular posts from this blog

Curriculum Vitae (C. V)

Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana. Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha. Ngoja ...