Skip to main content

Posts

Showing posts from July 19, 2017

NJOO NAE TUFURAHI

NJOO NAE TUFURAHI. Kwanza nawapa salamu, baba na mama pokeeni Kwa bashasha na hii hamu, kaka na dada hongereni Kwa kuhitimisha kaumu, watunzi wote poleni Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi Sasa hili kundi ni lako, litumie kwa usahihi Itume hadithi yako, Wimbo, shairi hata futuhi Vizuri usile kepeako, njoo nae tufurahi Njoo uimbe usome, njoo ucheke uburudike Kwa tungo zisizo ukame, njoo ujifunze uadilike Huu wigo wote tuungame, tulipokosa tuimarike Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi Kazi kwako ni moja, itimize usipuuze Ili tuongeze hoja, rafikizo uwaongeze Wajaze kwa kundi moja, wote kisha tuwapongeze Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi Writer: baraka ngeleja 0756775148

MAUMIVU

MAUMIVU Sili wala silali, ninakesha kama bundi Umenichoma msumari, haoung'oki hata kwa fundi Najua waona fahari, vicheko vyakutoka sundi Maumivu ndo jina langu, nipe pole salamu yangu Moyo wangu bado una jambo, nisikize mpenzi wangu Kwako nishanasha chambo, usisulubu mtima wangu Wengi wamekupa ulimbo, wakunase UA langu Maumivu ndo jina langu, nipe pole salamu yangu. Mangapi niliyapuuza, yalosemwa juu yako Leo mambo wayakuza, eti mie sio taipu yako Na vita unaitangaza, ama zangu ama zako Maumivu ndo jina langu, nipe pole salamu yangu. Kupenda hisani ya moyo, usiniumize mwenzio Hata fukara haki ninayo, rudi unitulize mwenzio Wakupao pesa wachoyo, wa penzi zaidi ya kileo Maumivu ndo jina langu, nipe pole salamu yangu Nauguza kidonda changu, unanitesa mpenzi wangu Hakuna raha tena kwangu, ebu tazama machozi yangu Vingi ulinizoesha wangu, chonde rudi hima kwangu Maumivu ndo jina langu, nipe pole salamu yangu. Ona watoto wanalia, subira imewaishia Majirani walokuzoe...