Skip to main content

NJOO NAE TUFURAHI

NJOO NAE TUFURAHI.
Kwanza nawapa salamu, baba na mama pokeeni
Kwa bashasha na hii hamu, kaka na dada hongereni
Kwa kuhitimisha kaumu, watunzi wote poleni
Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi

Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi
Sasa hili kundi ni lako, litumie kwa usahihi
Itume hadithi yako, Wimbo, shairi hata futuhi
Vizuri usile kepeako, njoo nae tufurahi

Njoo uimbe usome, njoo ucheke uburudike
Kwa tungo zisizo ukame, njoo ujifunze uadilike
Huu wigo wote tuungame, tulipokosa tuimarike
Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi

Kazi kwako ni moja, itimize usipuuze
Ili tuongeze hoja, rafikizo uwaongeze
Wajaze kwa kundi moja, wote kisha tuwapongeze
Vizuri usile pekeako, njoo nae tufurahi

Writer: baraka ngeleja
0756775148

Popular posts from this blog

Curriculum Vitae (C. V)

Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana. Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha. Ngoja ...