FATA MGANGA Asiyefuata funzo, nayo hekima hupotea Mjijini twapewa tuzo, Shauri yako utajaumbua Joto au baridi Senzo, Raggae danso twabanjua Kibamia sije mjini, fata mganga akuague. Fata mganga akuague, uje tembea mjini Huku njia uzikwangue, zote chocho, juu na kuni Mjini njia ulalue, ndefu, fupi na katini Kibamia sije mjini, fata mganga akuague. Mjini njia zote hupitika, tembea utakosa silidi Gari hupaki na kubanduka, Ilo bora au si maridadi Hata njia ilochoka, hubeba gari jadadi Kibamia sije mjini, fata mganga akuague. Mjini hakuna giza, mwangaza kote njiani Eti vibaka hufukuza, wasojiweza uwanjani Jeruhiwa kama funza, waendeshao pembeni Kibamia sije mjini fata, mganga akuague Mjini watoto huendesha, tena magari makubwa Mmoja atapoegesha, mwenza huramba ka mumbwa Trafiki naye unogesha, ruhusa gari kusombwa Kibamia sije mjini, fata mganga akuague. Mjini twawaona chura, wepesi kutikisa ntura Wasobabaika sura, hupagawi...