FATA MGANGA
Asiyefuata funzo, nayo hekima hupotea
Mjijini twapewa tuzo, Shauri yako utajaumbua
Joto au baridi Senzo, Raggae danso twabanjua
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague.
Fata mganga akuague, uje tembea mjini
Huku njia uzikwangue, zote chocho, juu na kuni
Mjini njia ulalue, ndefu, fupi na katini
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague.
Mjini njia zote hupitika, tembea utakosa silidi
Gari hupaki na kubanduka, Ilo bora au si maridadi
Hata njia ilochoka, hubeba gari jadadi
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague.
Mjini hakuna giza, mwangaza kote njiani
Eti vibaka hufukuza, wasojiweza uwanjani
Jeruhiwa kama funza, waendeshao pembeni
Kibamia sije mjini fata, mganga akuague
Mjini watoto huendesha, tena magari makubwa
Mmoja atapoegesha, mwenza huramba ka mumbwa
Trafiki naye unogesha, ruhusa gari kusombwa
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague.
Mjini twawaona chura, wepesi kutikisa ntura
Wasobabaika sura, hupagawisha hadhira
Huamini mwulize snura, mjini Ngosha anapura
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague.
Mji wajuaji wengi, hata pesa hawahitaji
Ufundi kuendesha Kwingi, kote utakuwa mtambaji
Tena ukiweka na tungi, hutoi hata ya bajaji
Kibamia sije mjini fata, mganga akuague
Mjini kibamia hakiliki, nani atatumbukiza mdomoni
Hata ukoleze kwa hiriki, radhaye hawaitamani
Mla tembo hana kiki, misuli kunogesha ndani
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague
Vicheko vitakuliza, njiani ukipita kapa
Rafikizo watakuuliza, mbona naniii kasepa?
Wasojua kunyamaza, husimanga ka'marapa
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague
Woga lulu ya jasiri, wakale walitwambia
Mjini hata rijali, humkwepa kibamia
Njia pana kuendesha gari, raha ukiwa na ngamia
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague
Kumi beti nahitimu, kibamia sio chuo changu
Usipoona umuhimu, baki shamba tu ndugu'angu
Kidagaa ulitia ngumu, unaweza kula hawa changu?
Kibamia sije mjini, fata mganga akuague.