Skip to main content

Posts

Showing posts from March 14, 2017

SAUTI KILINGENI

         SAUTI KILINGENI Baba na mama nawajia sikilizeni Wambie wanao pia "tulieni" KILINGENI sio mbali sana Tazama ile taa inawaka Punde si punde sote Tutaisikia sauti kama usikiavyo mauti Ikimjia aliyestahili Sio sauti ya vinanda ama shangwe Sio Sauti ya vifijo ama nderemo Sio Sauti ya vigelegele ama ngomezi Sio Sauti za mfu ama mtu hai Ni Sauti za kelele Kelele zilizozaa kelele za kale Waliochoshwa na ndwele za wakwele Waliojeruhiwa mwili mzima kwa mawe Ni Sauti zenye mpangilio wa haki Iliyogandamizwa na hao vigogo Wanaojiita wenye nazo Kutwa nzima kuwashurutisha wasonazo Wakiiba hisa na hisani zao Wakila wakashiba ndipo nao walemo Mabaki walobakizwa Sauti ya KILINGENI isikieni Hii Sauti sio huru nitumeni Imepita mingi bonde na mabondeni Vilindi na vikwazoni Msoweza kusikia isomeni Kote harufu ya zamu tena ni damu mbichi Walokufa ni haramu ila ni wananchi Tena huzikwa bila karamu mbali na nchi Ole atoaye chozi hat...