SAUTI KILINGENI
Baba na mama nawajia sikilizeni
Wambie wanao pia "tulieni"
KILINGENI sio mbali sana
Tazama ile taa inawaka
Punde si punde sote
Tutaisikia sauti kama usikiavyo mauti
Ikimjia aliyestahili
Sio sauti ya vinanda ama shangwe
Sio Sauti ya vifijo ama nderemo
Sio Sauti ya vigelegele ama ngomezi
Sio Sauti za mfu ama mtu hai
Ni Sauti za kelele
Kelele zilizozaa kelele za kale
Waliochoshwa na ndwele za wakwele
Waliojeruhiwa mwili mzima kwa mawe
Ni Sauti zenye mpangilio wa haki
Iliyogandamizwa na hao vigogo
Wanaojiita wenye nazo
Kutwa nzima kuwashurutisha wasonazo
Wakiiba hisa na hisani zao
Wakila wakashiba ndipo nao walemo
Mabaki walobakizwa
Sauti ya KILINGENI isikieni
Hii Sauti sio huru nitumeni
Imepita mingi bonde na mabondeni
Vilindi na vikwazoni
Msoweza kusikia isomeni
Kote harufu ya zamu tena ni damu mbichi
Walokufa ni haramu ila ni wananchi
Tena huzikwa bila karamu mbali na nchi
Ole atoaye chozi hatodumu
Ole ulizaye chanzo utapewa sumu
Sauti inatafutwa ili mbali kufutwa
Hata fadhira nilizokupa Leo unanitupa?
Msalia mtume hakosi ibadani
Ila mla nyama mpaka umchune ndo ataacha kisilani.
+255756775149