Skip to main content

AT 25 YEARS

LEO NAOMBA TUSHIRIKI JAMBO HILI:

Duniani kote miaka hii ya 2000 vijana tumekumbwa na changamoto kadha wa kadha. Mfano Ajila, Elimu na hata Malazi na Magonjwa (kwa kutaja chache). Hali hii imepelekea wengi kukosa muelekeo sahihi wa maisha na hata ndogo za wengi kufutikia gizani.

Kama kijana, yapo mambo mengi ambayo unapaswa kuyakamilisha au wakati mwingine kuwa nayo kabla umri ya ujana haujakuacha. Kumbuka siku zinasogea kwa kasi sana. Jiulize tuu hapo ulipo una miaka mingapi na baada ya miaka 5 ijayo utakua na mingapi. Hivyo basi zote ni changamoto ambazo tunapitia na tunatakiwa kuzishinda.

Pamoja na suala la elimu (ambalo si lazima sana) kijana unatakiwa kufanya yafuatayo kabla hujamalikisha miaka 25. Ni mambo matatu tu:

1. Uwe umeshawahi kufanya biashara: hapa haijalishi kama bado inaendelea au ulifanya biashara kisha mtaji na faida vikaporomoka. Kikubwa uwe umeshawahi kufanya biashara yako binafsi. Hii itakuwa imekusaidia kujua changamoto ambazo zipo katika biashara mapeeeema ukiwa na miaka 25. Tofauti na hivyo utakapotaka kufanya biashara above 25yrs itakupasa utafute Busness Consultants wakupe uelekeo.

2. Uwe umewahi kuishi angalau katika mji mkubwa mmoja nchi yoyote: Namaanisha uwe umewahi kuishi katika jiji au mji mkubwa kwa mfano Tanzania (Dar es salaam) Kenya (Nairobi) Nigeria (Lagos) n.k. Hii itakusaidia kufahamu changamoto zilizo katika mji/ jiji. Ukiwa umri wa miaka 25 tu utaweza kutembea na kufanya vitu vingi kwakua una uzoefu na miji mijubwa. Lakini pia kuishi mijini hata kama ni kwa muda tuu kutakusaidia kujifunza mengi ikiwa ni pamoj na mzunguko wa pesa na matumizi yake kama tujuavyo mijini kila kitu pesa hata ukitaka kuulizia duka la vipodozi liko wapi hahahaa. Tofauti na hivyo ukienda kuishi jijini kwa mara ya kwanza ukiwa above 25yrs kila kitu kitakua kipya kwako. Hali itakayokupelekea kupoteza pesa nyingi kwa matumizi yasiyo ya msingi.

3. Uwe umewahi kuwa katika mahusiano: Hapa kinachongaliwa ni kuwahi kuwa na mpezi au yawezekana bado unaye. Hii itakusaidia kwasababu utakua na uzoefu na masuala ya mahusiano. Kwa umri wa miaka 25 tuu unaweza kumshauri mtu juu ya mahusiano yake kwakuwa tayari na wewe ni muhenga. Tofauti na hivyo ni kuishia kutendwa, kujutia na kusaliti kila leo ukiwa above 25 yrs. Na wengi wanaosumbuliwa na mapenzi ni waleee walioanza wakiwa na umri zaidi ya miaka 25.

Huu ni mtazamo tuu na unaweza kukusaidia. Kama umeshazidi miaka 25 na hukuwahi kupitia hatua hizo tatu bado unaweza kufikia malengo na yawezekana tayari umeshafikia. Suala la msingi ni kuzidisha jitihada kwa kukabili challenges zilizopo katika mazingira yetu.

Good Luck Dears.

Popular posts from this blog

Curriculum Vitae (C. V)

Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana. Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha. Ngoja ...