NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
NGELEJA©UPP.
Kwa pesa au majumba ya kifahari mujini
Ama kumiliki shamba na ng'ombe wengi kijijini
Vipi kwa yangu kasumba kugawia pesa masikini
Swali lautesa moyo NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
Nimejaaliwa ucheshi je itakua kumbukizi?
Au kwa wangu ubishi fujo na hasira za mkizi
Uchoyo huwa sikopeshi na kiduchu kauwizi
Swali lautesa moyo NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
Je ni bora uongozi au uongozi bora
Kwa uzuri wa malezi ama kwa wingi ukora
Au ni uzuri wa mavazi na uanamitindo bora
Swali lautesa moyo NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
Sura yenye mvuto maulana kanijalia
Utanashati wa Vito na shepu ya kuvutia
Je kutembea kwa mnato na sauti inayovutia
Swali lautesa moyo NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
Kwa salamu maridhawa ambazo nakutumia
Au msaada wa ile dawa wakati umeugua
Je utaona sawa kunikumbuka kwa umbea?
Swali lautesa moyo NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
Ukimya nilouweka miaka hatujaonana
Siku sasa umezeeka je ndo tanikumbuka sana?
Umaarufu niloweka mitandaoni napatikana
Swali lautesa moyo NITAKUMBUKWA KWA KIPI?
Kwa wingi wawafuasi siku ya mazishi yangu
Au kwa kuongoza kuasi rafiki jamaa na ndugu
Kweli napata wasiwasi kipi ni kukumbukwa kwangu
Mora nijalie mema ili kwa mwema nikumbukwe.
Ngeleja©upp
0756775148