NI SALAMA KENYA.
Safari iso ndefu, leo mnaitimiza
Kama mbio za sakafu, ukingoni mwamaliza
Chagua iloturufu, kwa Kenya yenye mwangaza
Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza.
Chaguzi ni siku moja, mchague wa moyoni
Wala msilete vioja, kuivuruga amani
Sote ni ndugu moja, mnachagua rubani
Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza.
Kwa sala namwomba Mungu, alotuweka duniani
Wasitufitini wazungu, Afirika ina amani
Uchaguzi mwema wezangu, sisi kwenu majirani
Ni salama ni amani, Kenya tunaihimiza.
©UPP2017