Skip to main content

MONIKA

Mara ya kwanza nakutana na Monika ilikuwa mwaka 2014 nje ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akiwa analia kwa uchungu huku akisaidiwa na mume wake, monika alionekana kama mtu aliyekata tamaa kwa kukosa msaada. Walitembea taratiba kuelekea upande wa pili wa barabara lakini ghafla nikamwona Monika akianguka chini na mmewe akijaribu kumuinua huku na yeye akitokwa machozi. Ikanibidi niende kuwasaidia na tukaketi kwenye mgahawa jirani ili wapumzike kidogo.
Tukiwa hapo nikatamani sana kujua nini hasa kimewasibu ndipo Monika akaanza kunisimulia... "akasema wametoka kufanya checkup ya mfumo wa uzazi na daktari akamwambia hawezi kupata ujauzito katika maisha yake. Nilistuka kidogo lakini akaendelea kusema.... "ameishi na mume wake miaka sita pasipo kupata mtoto, wamejaribu kila aina ya dawa pasipo mafanikio, wameenda kwa waganga wengi lakini bado tatizo halikutatuliwa, wametumia pesa nyingi na hatimaye wakaamua kuja hapo hospitali ndipo wakaambiwa hawezi kupata ujauzito. kwakweli nilistuka sana na nikamtazama mme wake ambaye alikuwa na huzuni kubwaa. Ukiwa anaendelea kuzungumza, Monika akasema haya yote yanatokea maana akiwa kidato cha pili miaka kadhaa iliyopita aliwahi kutoa ujauzito ili aendelee na masomo yake ya sekondari tazama sasa anautafuta ujauzito kwa ghalama kubwa. Monika aliendelea kulia kwa uchungu mwingi akiwa amekata tamaa nakuona kama ndoa yake itapote.

Nikamwambia Monika yote haya ni matokea ya dhambi lakini yupo mmoja tu ambaye husafisha dhambi zetu na kutuweka huru. Ikiwa utakubali na kumtegemea yeye, atafungua uzazi wako nawe utapata watoto wengi wenye afya na familia yako itakuwa na furaha naye sio mganga wala huyo daktari Bali ni MUNGU MWENYEZI. Tulizungumza mengi kisha tukaachana, nao wakaelekea nyumbani.

Kwakuwa tulikutana na kuzungumza tu, hakuna kati yetu aliyekumbuka kuchukua namba za simu au mawasiliano zaidi ya majina wakati tunafahamiana.
Ila huwezi kuamini, tangu mwaka 2014 bila mawasiliano, lakini wiki hii kupitia mtandao wa facebook, niliona friend request jina Monika baada ya kukubali nikaona inbox picha kama 15 za mtoto. Nikastuka lakini baadae kidogo akatuma ujumbe na akijatambulisha kwangu kuwa yeye ndiye monika yule wa Muhimbili.

Nashukuru Mungu nilikumbuka haraka na akaniambia huyo ni mtoto wake wa kiume anaitwà Praise ana umri wa mwaka mmoja. Tuliongea mengi sana na akaniambia tangu siku ile walianza kumwomba Mungu na kumtegemea yeye wala haikuchukua muda akapata ujauzito. Hakika hakuna lisilowezekana kwa mungu wetu.

Kama unaamini hivyo, type Ameni kisha share kwa rafiki zetu ili wasibabaishwe na yale yaliyo mepesi kwa Mungu.

Ubarikiwe wewe na Familia yako.

        Contact..... 0756775148

Popular posts from this blog

Curriculum Vitae (C. V)

Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana. Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha. Ngoja ...