Sehemu ya pili tuliona vipengele vya Education background/qualification na Work Experience, Leo tumalizie vipengele vingine muhimu katika uandaaji wa C. V.
4. Training.
Hapa unapaswa kuandika mafunzo yote ambayo umeyapitia kwa kuzingatia mwaka yaani unaanza na recent training to old. Usisahau kuandika taasisi au chama kilichotoa training hiyo.
5. Awards and Achievement
Katika sehemu hii unapaswa kuandika awards mbali mbali ambazo umewahi kutunukiwa. Inaweza kuwa shule ni, chuoni, kazini ama sehemu yoyote inayotambulika. Unapoweka award hiyo kumbuka ni lazima uwe na uthibitisho yaani cheti. Utaratibu wa uandishi ni kuanzia na recent to old.
6. Skills
Sehemu muhimu sana na huangaliwa kwa jicho pevu wakati wa kuomba kazi. Hapa utaandika stadi zako na ujuzi ulionao, mfano lugha, reading, writing, computer, administration skills na kadhalika. Kumbuka unapoandika skill usiyonayo ni hatari kwa C. V yako.
7. Membership
Katika sehemu hii unatakiwa uandike kama wewe ni member wa taasisi au organization yoyote ile. Kumbuka kuandika na cheo chako au wajibu wako.
8. Publication
Sehemu hii sio ya kila mtu, Bali ni kwa wale waandishi tu. Unatakiwa kuandika kazi mbakimbali ambazo umechapisha au hata ambazo hujachapisha yaani unpublished. Itakuongezea credit katika C. V yako.
9. Hobbies and Interests
Katika sehemu hii utaandika vile uvipendavyo kwa ufupi tu na kuvitaja. Mfao swimming, jogging, Reading, Watching TV shows etc.
10. Referee
Hapana sasa, unatakiwa kusema watu ambao wataweza kusema juu yako. Watu hao ni lazima wawe wanakufahau vizuri na unashauriwa uwe umewapa taarifa kwamba ndio referee wako. Kwa kawaida watu hao wasizidi watatu na wasipungue wawili.
********************
Ushauri.... 0756775148