Katika sehemu ya kwanza tumeona maana ya wasifu binafsi ama C.V na tukaangalia sehemu muhimu inayoeleza Maelezo binafsi (Personal Particular).
Tuendelee na sehemu zingine muhimu:
2. Educational Qualification/Background (Taarifa za Elimu).
Sehemu hii unapaswa kuandika taarifa zako za elimu tena kwa umakini sana. Hapa andika shule na vyuo vyote ambavyo umepata kusoma na kuhitimu. Unashauriwa kuandika kwa kuanza na Kiwango kikubwa cha elimu mpaka lile kidogo yaani lile kiwango ulichomalizia Mpaka ulichoanzia ambacho ni Primary Education au O-level Secondary education. Kumbuka kuandika mwana na qualification ama kwa nina lingine certificate. Hapa ni sehemu muhimu sana inayotazamwa na mwajiri wako. Tuataona mfano hapo badae.
3. Work Experience (Uzoefu kazini).
Unapotazama job vacant kwa asilimia mkubwa wanahitaji mtu mwenye uzoedu ili wamwajili. Ni kweli bila uzoefu hakuna kazi, hivyo wewe kama mwombaji ni lazima uwe makini kuandika sehemu hii ili usipoteze sifa yako. Kumbuka kazi ambazl umewahi kufanya sehemu tofauti tofauti zilizo rasmi kisha andika kwa kuanza iliyo ya hivi karibuni mpaka ile ya zamani au uliyoanza kuifanya. Andika kwa ustadi zaidi ili kuvutia anayeisoma C.V yako.
Kipengele hiki hupaswi kukiacha wazi, na hii imekua ni swali ama mjadala hasa kwa wale wanaomaliza masomo yao na kutafuta ajira. Kumbuka unaweza kuandika uzoefu wako hata kwa kuzingatia mafunzo kwa vitendo ambayo umewahi kufanya wakati upo masomoni lakini pia utaweza kuandika ikiwa uliwahi kufanya temporary work sehemu yoyote. Hupaswi kuacha wazi.
Itaendelea...........
Ushauri.... 0756775148.