Sehemu 01.
BAHATI ni Kijana wa pekee katika familia ya Mzee Mkuti. Kijana huyu akiwa darasa la pili tayari alikuwa ameshaanza kuchunga mifugo ya baba yake kama vile mbuzi na kondoo. Alifanya kazi hiyo kila siku za jumamosi na jumapili ambapo anakuwa haendi shuleni. Mama yake alimpenda sana bahati na Mara nyingi Kabla hajaenda kuchunga aliandaliwa viazi na Karanga za kutosha ili atumie anapokuwa kwenye machungo, Mama alipenda kumkumbusha bahati kuchukua maji ya kunywa maana jua kali huleta kitu cha maji na sehemu anayoenda kuchunga hakuna makazi ya watu. "Mwanangu umekumbuka kubeba maji ya kunywa ya kutosha?" Aliuliza Mama kila siku ambayo Bahati alikua akitoa mifugo zizini tayari kwenda kuchunga.
Bahati aliipenda sana kazi ya kuchunga kwa sababu alikuwa mvivu wa kuchota maji na kutafuta kuni nyumbani. Hivyo akijitahidi kuwahi kuondoka asubuhi na mapema ili asibadilishiwe kazi. Akiwa machungani Bahati alipenda kupanda huu ya miti ya mapera na maembe, mara chache alikutana na vijana wengine ambayo nao walikuwa wakichunga mifugo hao.
Siku moja akiwa machungani, BAHATI alishtuka sana baada ya kuhisi nywele zake zinasisimuka na akahisi kutetemeka. Kwa mara ya kwanza, Bahati alijawa hofu na akagundua pale sio sehemu salama tena, hivyo akajaribu kukusanya mifugo yake ili atoweke sehemu ile. Akiwa anaendelea kukusanya mbuzi ambao wana kawaida ya kutawanyika huku na kule, BAHATI alikumbuka hadithi aliyowahi kusimuliwa na babu yake kuhusu Mazimwi na majitu ya kutisha yaliyowahi kutokea katika kijiji chao miaka mingi iliyopita, lakini pia alikumbuka jinsi babu yake alivyomtahadhalisha kutembea msituni nyakati za jua Kali kwani viumbe wabaya nao hutembea kwa kutafuta maji na chakula Wakati huo. Kumbukumbu hizo zilimtia hofu bahati ambaye tayari alikuwa peke yake polini na mifugo ambayo wametawanyika kila sehemu. Alipokuwa akijitahidi kukusanya mbuzi na kondoo wake, Ghafla akaona nyoka wawili waliokuwa wakipigana, mmoja alionekana mdogo na mwingine mkubwa. Katika kupiga na yule mdogo alipigwa na kupoteza fahamu kisha yule mkubwa alienda sehemu akachuma majani na kumpulizia nyoka mdogo nae alipata fahamu kisha wakaendelea kupigana. Walifanya hivyo mara kadhaa kitendo ambacho kilimfanya bahati agundue kumbe yale majani ni dawa ya kumtibu nyoka. "Nitaenda kumwambia babu nimeijua dawa ya kumponya nyoka, najua babu atafurahi sana", aliwaza. Bahati alifikiria kitu akilini mwake "je Nikichukua nyoka mdogo nikampeleka nyumbani mama atanipiga? Akinipiga nitamficha..... Lazima nimfuge nyoka huyu maana bado ni mdogo sana ndio maana anapigwa. Au ataniuma?"
Itaendelea jumamosi ijayo.
Ushauri... 0756775148.