Skip to main content

NEEMA: "NISAMEHE MAMA".

   NEEMA: "NISAMEHE MAMA".

SEHEMU 01.

Wakati baba yake NEEMA anaaga dunia, Neema alikuwa tumboni mwa mama yake akiwa na umri wa miezi sita. Msiba wa Mzee Kajumba uliwahuzunisha wengi hasa kutokana na sababu kuwa Mzee Kajumba alikuwa mcheshi na kiongozi makini mwenye kujali demokrasia katika kijiji cha Sarando.
Mzee Kajumba alipatwa na mauti siku ambayo alikuwa na baadhi ya rafiki zake kwenye kilabu cha pombe kwa Mzee Nzukwa. Baada ya kupata kinywaji hicho, aliamua kuwaaga wenzake ili arejee nyumbani mapema. Ilikuwa saa mbili usiku, na wazee hawa walizoea kurudi nyumbani kuanzia saa nne na wakati mwingine mpaka saa tano usiku.
Siku hiyo, Wenzake walimshauri awasubiri ili waende pamoja ila Mzee Kajumba alikataa hivyo akaanza safari kurudi nyumbani huku akiimba wimbo alioupenda siku zote. Ni wimbo wa kumsifia mke wake Bi Tausi ulioimbwa:

  Mzuri ni wewe tausi wanguuu
Moyo wangu umekukumbuka tausi wanguu
  Nakuja nyumbani mama tausi wanguu
  Nione uzuri wako tausi wanguuuu...

Alirudia wimbo huo mara kadhaa kadri fikra za kumkumbuka mke wake zilipomjia. Wakati alipoendelea kutembea huku akiweweseka kwasababu ya kulewa, ghafla kimvua kikaanza kunyesha na mara ikawa mvua kubwa. Mzee Kajumba hakuona haja ya kujibanza sehemu ili asubiri mvua iishe bali aliendelea kutembea kwenye uterezi na matone makubwa ya mvua yalimlowanisha mwili mzima.
Hakuweza kuona tena nini kipo mbele yake huku mwanga wa radi uliojaribu kumsaidia kuelewa anapoweza kupita lakini bado haikusaidia kitu. Mzee Kajumba hakuweza kuimba wimbo wake tena zaidi alianza kuhisi hali ya hatari ikimnyemelea mbele yake.
Alitereza na kuinuka mara kadhaa hali ambayo ilimfanya akose nguvu na hata kusukumwa na maji yaliyopita kwa kasi. Mzee Kajumba hakuweza kuongea wala kupiga kelee kwasababu ya baridi na upepo mkali uliozidisha kasi ya matone ya mvua usiku huo. Ghafla alitereza na akasukumwa na maji yenye kasi zaidi mpaka mtoni. Hakuweza kuogelea kutokana na uchovu hivyo alisubiri kifo kimpate tu. Mzee Kajumba alimkumbuka mke wake kipenzi Tausi, alikumbuka ujauzito aliotamani amshuhudie mtoto wake wa kwanza, baada ya kuhangaika kwa miaka sita bila mafanikio ya kumpata mtoto mpaka pale walipompata mganga wa jadi aitwaye Nyizungwatu kutoka kijiji cha tatu ndipo walipofanikiwa. Pia Mzee kajumba alikumbuka ushauri wa marafiki zake kule kilabuni kwamba wasubiriane ambao labda ungemuepusha na madhira anayoyapata ila yeye akakaidi, kisha akaikumbuka ahadi yake kwa mke wake kwamba akijifungua mtoto wa kike atampatia zawadi nzuri ambayo aliiandaa kila siku na alifanya siri wala Bi tausi hakuwa anajua ni zawadi gani hiyo. Alilia kwa uchungu sana na baada ya kufikiri hayo yote hatimaye akakata roho...

           Itaendelea  juma tatu ijayo..

    Jiaandae kufuatilia mfulululizo simulizi nyingine itakayoanza wiki hii ijumaa inayoitwa "Fall Of Drugs Forts (Kuangushwa kwa Ngome ya madawa ya kulevya)".

   Ushauri.... 0756775148.

Popular posts from this blog

Curriculum Vitae (C. V)

Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana. Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha. Ngoja ...