Skip to main content

NEEMA: NISAMEHE MAMA ... 02.

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA.....Mzee Kajumba alishindwa kupambana na dhoruba Kali ili kuokoa maisha yake, hatimaye Akakata roho,,,, je nini kitaendelea Wakati Kyle nyumbani mkewe hajui lolote??????
ENDELEA.........

Usiku huo Bi tausi hakuwa na raha kabisa ndani ya chumba chake cha tofari za udongo ambacho kimeezekwa na nyasi. Alijaribu kutoka nje ili aone labda Mzee kajumba atakuwa amefika lakini upepo mkali haukumpa nafasi kutoka nje hivyo alijaribu kuchungulia tu wala hakuweza kuona mbele sababu ya giza kali. Akajisemea moyoni mwake 'huenda atakuwa kwa rafiki yake Bwana Juma'. Lakini haikuwa kawaida ya Mzee kajumba kuchelewa kiasi hicho jambo ambalo liliendelea kumpa wasiwasi. Aliendelea kumsubiri mme wake kipenzi mpaka usingizi ukamchukua akiwa amekaa kwenye kiti cha marimba ndani ya chumba chake.
Wakati usingizi unamwachia Bi tausi ilikuwa yapata saa tisa na nusu usiku. Alipoamka hakumwona mme wake ikabidi apate hofu zaidi, bila kujali usiku aliamua kutembea mpaka kwa Mzee juma ikiwa ni kama kilomita mbili hivi. Alipofika akabisha hodi mara kadhaa ndipo sauti ya bwana juma iliitika kwa chini. Alikaribishwa ndani huku kukiwa na hofu kubwa ndipo bi tausi aliuliza kama mme wake yupo pale wakati huo. Bwana juma alistuka baada ya kusikia swali hilo ndipo akamwelezea kisa chote kule kilabuni na jinsi mzee kajumba alivyowahi kurudi nyumbani. Bi tausi alipata mshangao wakati machozi yakimtiririka mashavuni, alifikiri jinsi mzee Kajumba alivyomuaga huku akiahidi atawahi kurudi, mmewe alipenda kumtania hasa tangu awe na ujauzito na maisha yao yalitawaliwa furaha na bashasha za aina hiyo.
Huku wasielewe cha kufanya, waliulizana je atakuwa wapi? 'Hapa kijijini hakuna wanyama wakali.. Alisema Bi tausi. "Itabidi twende kwa mjumbe tukatoe taarifa ili filimbi ipulizwe tumtafute ... Alishauri Bwana juma. Waliondoka mpaka kwa mjumbe na baada ya kumpa taarifa hivyo alistuka na kusema ''lazima kuna tatizo limemkumba, Mzee kajumba si mtu wa kupotea kwake''. Mjumbe alimwamuru kamanda apulize filimbi ili kijiji kijue kuna tatizo kabla haijawa alfajiri, ndipo baada ya dakika ishirini na tato tu, zaidi ya robo tatu ya wanakijiji walifika kwa mjumbe. Walipewa taarifa na wakamua kumtafuta usiku huohuo mpaka apatikane Mzee kajumba.
Walitawanyika na kupeana ishara iwapo kama ikitokea kubainika tatizo, na ilipofika saa mbili asubuhi kijiji chote kilikuwa na vilio pamoja na majonzi baada ya kuukuta mwili wa mzee kajumba ukielea kwenye mto uliokua jirani na kijiji cha pili. Bi tausi baada ya kufahamu mume wake amefariki dunia alipoteza fahau na majirani wakampeleka kituo cha afya ili apate huduma ya Kwanza

      Je, Bi Tausi nae ataaga dunia? Vipi kuhusu Ujauzito alionao? Kwakuwa Mzee Kajumba Tayari ameshafariki nini kitafatia Wakati mkewe akiwa hospitalini? USIKOSE KUFATILIA SIMULIZI HII JUMATATU IJAYO.......

      Maoni na Ushauri..... +255756775148.

Popular posts from this blog

Curriculum Vitae (C. V)

Jana nilifika katika kituo kimoja cha afya na katika Harakati za hapaaaa na pale, nikiwa nimekaa kwenye benchi ili nipumzike kidogo. Nikiwa pale wakatokea wauguzi wawili nao wakakaa karibu yangu na wakaanza kuzungumza. Mmoja akamwambia mwenzake juu ya changamoto za ajira na jinsi alivyojitahidi kutafuta nafasi hata za kujitolea bila kufanikiwa, na yule mwenzake nae akamwambia jinsi alivyopambana mpaka kupata nafasi hiyo japo wanalipwa ila bado ni posho kidogo sana. Sasa, katika mazungumzo yao mwanzoni hayakunihusu japokuwa niliyasikiliza Si unajua tena sikio halina mlango lakini walifikia kipindi wakanishirikisha kwa namna moja ama nyingine hasa walipoanza kujadili vikwazo walivyokutana navyo. Ni vikwazo vingi ila hivi viwili vitakuhusu hata wewe pia. Wakisema cha kwanza ni kuandika barua ya kuomba ajira ama kujitolea na ilitakuwa iandikwe kwa lugha ya kiigereza na kingine ni kuandaa wasifu binafsi (c.v) inayoonesha mtiririko mzuri wa taarifa zako. Hapo sasa wakanishirikisha. Ngoja ...