THE DOWNFALL OF DRUGS FORT.
(Kuanguka kwa ngome ya madawa ya kulevya)
"Kijana njoo tafadhari" Ilikuwa ni sauti ya mwanaume aliyeongea baada ya kushusha kioo cha gali lake jeusi aina ya V8. Nakumbuka ilikuwa ni jumatano asubuhi ambapo kama kawaida nilipenda kwenda Manzese darajani kusoma magazeti labda nitabahatisha nafasi ya ajira.
Baada ya kusikia sauti hiyo na kujiridhisha kwamba Mimi ndiye naitwa, niliamua kusogelea gali ile.
"Vipi unahitaji kazi?" Aliuliza.
"Ndiyo brother nahitaji na hata hapa ninaangalia kurasa za magazeti kama nitapata tangazo la nafasi za kazi" Nikijibu kwa mfululizo kama nimeulizwa ninafanya nini mahali pale.
"Ingia ndani ya gali tuongee kijana" Akisema nami nikatii na kuingia ndani ya gali lake hilo.
"Naitwa Mr SUNi, Mimi ni mfanyabiashara hapa jijini na nina biashara tofauti tofauti zenye kuingiza pesa nyingi sana" Alijieleza
"Naitwa CHIDO" Nilijibu kwa hofu huku nikiangalia pembeni Wakati huo Mr. SUNi akinikazia macho na akionekana mtu wa kutisha.
"Jisikie huru kijana upo sehemu salama, okay?"
"Ndiyo brother nipo huru" Nilijibu na kujilazimisha kucheka.
"So, tunaweza kuondoka Kwa mazungumzo zaidi na kufahamiana pia?" Aliuliza nami nikakubali.
Hivyo tuliondoka na kuelekea Sinza mtaa wa MoRi ambapo Wakati tukiwa njiani Mr SUNi aliendelea kunitoa hofu na kunisifia jinsi nilivyo kijana jasiri.
"Una elimu gani CHIDO?" Alihoji
"Nimehitimu degree ya uongozi wa biashara katika chuo kikuu cha Mlimani, lakini ndiyo hivyo ajira hakuna mtaani" Nilijibu huku nikijaribu kutabasamu na muda huo Mr SUNi alikua bize akiendesha gali.
"Hahahahaa" Alicheka kisha akasema... Ajira zipo sana ila tatizo vijana wengi sio majasiri na wanapenda kazi za ofisini tuuuu, viti vya kuzunguka, na wanawaza magari, majumba eeeh" Alisema Mr SUNi na kunifanya nipate hofu juu ya kazi ninayoenda kuipata muda Si mrefu, je itakuwa na maslahi kweliii?
Tuliendelea na safari mpaka tukafika mbele ya Jumba nzuri la kifahari na aliposimamisha gari tu geti likafunguka na tukaingia ndani. Kilichonishangaza baada ya kuingia ndani na kushuka kwenye gali tayari tulikua sebureni, nikajaribu kuangaza kumbee lile gali liliingia mpaka ndani ya nyumba na ndimo parking yake ilipo, mmmh!!! Ama kwelii watu wanapesa nchi hii.
"Karibu sana CHIDO, hapa ndiyo nyumbani kwangu" Alinikaribisha nami nikajibu asante. Nilindelea kushangaa furnitures zilizoipamba Jumba lile la thamani, Wakati huo Mr SUNi akifungua jokofu na kutoa vinywaji kwisha akanipatia na tukagonga cheers.
"Kama nilivyosema awali, wewe ni kijana jasiri sana na unapaswa kumiliki pesa nyingi na biashara zako Kubwa, so I want to make you rich na utafanikiwa Sana" Aliongea Mr SUNi huku akiniangalia usoni.
"Nitafurahi sana brother na hiyo ndio ndoto yangu siku zote" Nilijibu huku nikitaka kupiga magoti kushukuru lakini alinizuia.
"Anyway, sisi tupo wengi katika biashara zetu, its an organization, na sote tuna pesa nyingi, kama utakua tayari itabidi nikukutanishe na mkuu wetu ili tufanye contracts na malekezo mengine"
"Nipo tayari kuanza hata muda huu" Nilijibu hivyo pasipo kujua ni biashara au kazi gani nitaanza kuifanya na kundi hilo, je itakua na faida kiasi gani.
"Okay let me call him" Alisema Mr SUNi huku akitoa simu mfukoni na Mara bastola ikaanguka chini.......
Itaendelea jumapili ijayo
Ushauri..... 0756775148